Categories
Nasaha za leo

MADHAMBI NI KIZUIZI CHA KUFANYA WEMA

قال ابن القيم رحمه الله تعالى عن آثار الذنوب: (( فينقطع عليه بالذنب طاعات كثيرة، كل واحدة منها خير له من الدنيا وما عليها. وهذا كرجل أكل أكلةً أوجَبَتْ له مرضة طويلةً منعته من عدة أكَلات أطيب منه

Amesema Ibnu Alqayyim, Allah amrehemu kuhusiana na athari mbaya ya Madhambi: [[ Matendo mema yaliyo mengi mno hukatika (yaani hawezi kuendelea kuyafanya) kwa sababu ya madhambi (aliyoyafanya), kila mojawapo katika hayo mema yaliyokatika ni bora zaidi kwake kuliko dunia na vilivyomo juu yake. Na huyo mtendaji wa dhambi ni mfano wa mtu ambaye amekula chakula fulani (kibaya) kikamsababishia maradhi ya muda mrefu mno, chakula hicho kikamzuia na vyakula mbalimbali vilivyo vizuri sana kuliko hicho (kibaya). ]]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *