Categories
Nasaha za leo Picha/Kadi

Kuna baadhi ya watu ambao wanaamini kwamba mkosi upo kwa watu au eneo, na wanadhani kwamba shari inaweza kuwapata kutoka katika maeneo hayo au watu hao moja kwa moja pasina hukumu ya Allah na makadirio yake. Na hii ndio imani ya mkosi ambayo Mtume swallallaahu alaihi wasallam ameikataza na akaeleza kuwa ni ushirikina. Kwa sababu mwenye imani ya mkosi anaamini kwamba kilichompata katika mabaya kinatoka kwa viumbe kama vile wakati au eneo au mtu, matokeo yake anamchukia mtu huyo au wakati huo au eneo hilo na anajitenga mbali nalo akidhani kwamba ndilo limemletea shari na anasahau au kujisahaulisha kuwa hakika kilichompata ni kutokana na hukumu ya Allah na makadirio yake na kwa sababu ya dhambi zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *