Categories
Nasaha za leo

CHUKUA MWONGOZO HUU LEO

Amesema Ibnu Abdi Albarry ALLAH amrehemu: [ Ilikuwa ikisemwa kwamba, mambo sita yakidharaulika (na watu wakayafanya) basi wafanyaji wasizilaumu isipokuwa nafsi zao:-

(1) Mwenye kwenda katika meza ( mwaliko) ambao hakualikwa.

(2) Mwenye kutafuta fadhila (kukirimiwa) na mtu bakhili (mchoyo).

(3) Na mwenye kuingilia maongezi kati ya watu wawili pasina wao kumuhusisha.

(4) Na mwenye kumdogesha kiongozi.

(5) Na mwenye kukaa kikao asichostahiki.

(6) Na mwenye kumzungumzisha asiyemsikiliza wala kuyaelewa mazungumzo yake.]

IMETARJAMIWA KUTOKA KITABU AL ADAAB AASH-SHAR'IYYAH LIBNI MUFLIH UKURASA 347

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *