Categories
Nasaha za leo

UHALISIA WA NEEMA NA TABU ZA DUNIANI

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللّهِ صلى الله عليه وسلم : ” يُؤْتَى بِأَنْعَمِ أَهْلِ الدُّنْيَا ، مِنْ أَهْلِ النَّارِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ، فَيُصْبَغُ فِي النَّارِ صَبْغَةً : ثُمَّ يُقَالُ : يَا ابْنَ آدَمَ هَلْ رَأَيْتَ خَيْراً قَطُّ ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ نَعِيمٌ قَطُّ ؟ فَيَقُولُ : لاَ ، وَاللّهِ يَا رَبِّ . وَيُؤْتَى بِأَشَدِّ النَّاسِ بُؤْساً فِي الدُّنْيَا ، مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ ، فَيُصْبَغُ صَبْغَةً فِي الْجَنَّةِ ، فَيُقَالُ لَهُ : يَا ابْنَ آدَمَ ! هَلْ رَأَيْتَ بُؤْساً قَطُّ ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ شِدَّةٌ قَطُّ ؟ فَيَقُولُ : لاَ ، وَاللّهِ يَا رَبِّ ، مَا مَرَّ بِي بُؤْسٌ قَطُّ ، وَلاَ رَأَيْتُ شِدَّةً قَطُّ ” .

Kutoka kwa Anas Ibn Maalik Allah amridhie amesema, Amesema Mtume swallallaahu alaihi wasallam:
[ Ataletwa siku ya Qiyama mtu aliyeneemeshwa zaidi kuliko watu wote wa duniani, ambaye ni miongoni mwa watu wa motoni; ataingizwa katika moto mara moja tu, kisha ataulizwa “Ewe mwanadamu Je, ulishawahi kuona kheri yoyote kamwe? Je, ulishawahi kupitiwa na kheri yoyote (duniani)? Atasema, ‘Hapana , Wallaah; ewe Mola wangu!’ Na ataletwa mtu aliyetaabika zaidi kuliko watu wote wa duniani, (naye) ni miongoni mwa watu wa peponi, ataingizwa peponi mara moja tu , kisha ataulizwa; “Ewe mwanadamu, Je ulishawahi kuona tabu yoyote? Je, ulishawahi kupitiwa na shida yoyote (duniani)? Atasema, ‘ Hapana, Wallaah; ewe Mola wangu, sikuwahi kupitiwa na tabu yoyote , wala sijawahi kuona shida yoyote.]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *