Categories
Nasaha za leo

KUFANYA JITIHADA KATIKA NJIA YA ALLAH


قَالَ ابن القيم رحمه الله تعالى عن قوله تعالى: (( وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا)), علق سُبْحَانَهُ الْهِدَايَة بِالْجِهَادِ فأكمل النَّاس هِدَايَة أعظمهم جهادا وأفرض الْجِهَاد جِهَاد النَّفس وَجِهَاد الْهوى وَجِهَاد الشَّيْطَان وَجِهَاد الدُّنْيَا فَمن جَاهد هَذِه الْأَرْبَعَة فِي الله هداه الله سبل رِضَاهُ الموصلة إِلَى جنته

Amesema Ibnu Alqayyim Allah amrehemu, kuhusu kauli ya Allah ifuatayo; (( Na wale watakaofanya jitihada kwa ajili yetu tutawaongoza katika njia zetu)) ; Al-a’nkabuut 69.
[ Allah Mtukufu ameegemeza uongofu katika jitihada; hivyo basi, mwenye uongofu uliokamilika zaidi kuliko watu wengine ni yule mwenye jitihada kubwa zaidi (katika njia ya Allah) kuliko wengine. Na jihadi (jitihada) ya faradhi zaidi ni Jihadi ya nafsi, na Jihadi ya matamanio na Jihadi ya shetani na Jihadi ya dunia. Yeyote atakayefanya jitihada katika hayo manne kwa ajili ya Allah , Allah atamuongoza katika njia za ridhaa yake zenye kumfikisha katika pepo yake. ]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *