دخل رجل على سلمان الفارسي رضي الله عنه وهو يعجن!
فقال: ما هذا يا أبا عبدالله؟
Aliingia bwana mmoja kwa Sulaymaan Al-faarisiy Allah amridhie akamkuta akiwa anakanda unga , akasema : Kipi hiki ewe baba Abdullah ( kwa kipi unafanya kazi mwenyewe ) ?
قال: بعثنا الخادم في عمل فكرهنا أن نجمع عليه عملين
Akasema : “Tumemtuma mfanyakazi wetu katika kazi fulani na tukachukizwa kumkusanyia juu yake kazi mbili.”
Nimesema :
Hivi ndivyo walivyokuwa wema waliotangulia na watumishi wao , wakiwapa nafasi ya udugu na kuwafanyia muamala wa upole bali na kuwasaidia majukumu, nasi tunasema kama alivyosema Mtume wa Allah kuwaambia waliopewa nafasi ya kuwa na wasaidizi wa kazi :
” Hawa ni ndugu zenu na Allah amewajaalia kuwa mikononi mwenu , msiwape kazi wasizo ziweza na mkiwapa kazi basi wasaidieni. “