Categories
Nasaha za leo

UKARIMU SI KWA KUMILIKI KIKUBWA

Amesema sheikh Muhammad bin ghaalib Al-umariy Allah amuhifadhi :


لا يشترط لكي تكون كريما أن تكون غنيا. فقد تجد فقيرا معدما من أكرم الناس، بل ومن أسرعهم مبادرة لمساعدة المحتاجين، ومن أعفّهم عن السؤال.


(( Hakuna shart ili kuwa mkarimu uwe tajiri , hakika unaweza kumkuta fakiri asiyekuwa na kitu lakini ni katika watu wakarimu zaidi bali ni miongoni mwa wenye kufanya haraka kuwasaidia wenye uhitaji , na ni katika watu waliojizuwia zaidi na kuomba ,

وعلى العكس قد تجد غنيا، لكنه من أبعد الناس عن الكرم، بطيئا في الإنفاق، سريعا في المنع منه.


Bali pia kinyume chake unaweza kumpata tajiri , lakini ni katika watu walio mbali na ukarimu , mwenye kujiweka nyuma katika kutoa , mwepesi wa kuzuwia.))

Nimesema :

Kwa kutoa katika mahitajio ya ndugu zako na kusimamia kwako mambo ya dini kwa Mali yako hakuna kinacho pungua katika mali yako bali ni jambo la kuitia baraka Mali yako

hakuna ulazima katika utoaji kutoa kikubwa wala wenye kikubwa ndio watoaji na wenye vidogo hawatoi mpaka wawe na vikubwa na vingi laa

bali shiriki katika kutoa kwa kadri ya nafasi yako na jitahidi kujiweka mbali na kuhesabu na ubakhili hakika ukarimu ni tabia kama ulivyo ubakhili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *