Categories
Nasaha za leo

MWEZI WA ALLAH MUHARAM

Bado tupo katika miezi mitukufu mitatu yenye kufuatana na huu ni mwezi wa muharam ambao umeegemezwa kwake kwa kuitwa شهر الله المحرم Mwezi wa Allah wa muharam

Katika miezi hii mitukufu Allah subhaana wataala amesema :
فَلا تَظْلِمُوا فِيْهِنَّ أَنْفُسَكُمْ
Basi msizidhulumu ndani yake nafsi zenu

Amesema Ibnu Abaas Allah amridhie:
فجعلهن حراماً وعظّم حرماتهن، وجعل الذنب فيهن أعظم، والعمل الصالح والأجر أعظم.
Akaifanya miezi kuwa mitukufu na akaukuza utukufu wake , na akajaalia dhambi katika miezi hio kuwa kubwa zaidi na matendo mema na ujira kuwa mkubwa zaidi

Na akasema Qataada Allah amrehem :
فعظموا ما عظم الله، فإنما تُعظّم الأمور بما عظمها الله به عند أهل الفهم وأهل العقل.
Yatukuzeni yale ambayo Allah ameyatukuza , kwa hakika hutukuzwa na kupewa nafasi kubwa mambo kwa yale ambayo Allah ameyatukuza kwa watu wenye ufaham na akili
( تفسير ابن كثير رحمه الله: تفسير سورة التوبة آية 36).

MIONGONI MWA MATENDO BORA KATIKA MWEZI HUU WA MUHARAM

kukithirisha kufunga ndani ya mwezi huu

Amesema Mtume swallah Allahu alaihi wasalam:

أفضل الصّيام بعد رمضان شهرُ الله المحرم
Funga iliokua bora baada ya funga ya ramadhan ni funga katika mwezi wa Allah wa muharam

 (رواه مسلم 1982)

Amesema ibn Uthaimin Allah amrehem:
ولكن قد ثبت أن النبي صلى الله عليه وسلم لم يصم شهراً كاملاً قطّ غير رمضان،
lakini imethibiti kwa Mtume wa Allah hakufunga mwezi mzima kamiki kinyume na ramadhan
فيحمل هذا الحديث على الترغيب في الإكثار من الصّيام في شهر محرم لا صومه كله.
Basi itabebwa hadith hii na kupewa hukmu ya himizo la kukithirisha kufunga mwezi wa muharam na sio kuufunga wote

hivyo basi tukithirishe ndani ya mwezi huu ibada ya funga pamoja na kuchunga kuingia katika madhambi kwani madhambi ndani ya miezi mitukufu ni makubwa zaidi na tupupie kheri kwani ujira wa kheri ndani yake ni mkubwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *