Categories
Nasaha za leo

USIWE MSAADA KWA SHEYTWAAN

                            عن ابن مسعود -رضي الله- عنه قال: 

    Kutoka kwa Ibn Mas’uud Allah amridhie amesema :-

“إذا رأيتم الرجل منكم قارف ذنبا، فلا تدعوا الله عليه، ولا تسبوه، ولكن ادعوا الله أن يعافية”

 (( Pindi mtakapo muona ndugu yenu ameyaingia madhambi , basi msimuombee kwa Allah dhidi yake , wala msimtusi , lakini muombeeni kwa Allah amsalimishe  kutokana na madhambi hayo )).

[التوبة لابن أبي الدنيا (99)]

Nimesema :

 Sisi tuna wajibu wa kuhakiki mapenzi kati yetu na kuziokoa nafsi zetu na za jamaa zetu kutokana moto wa Allah na kamwe hatupaswi kusema hawatuhusu au kuridhia wanayoyafanya katika madhambi au kuwaombea upotevu huku ni kumsaidia na kumfurahishwa Sheytwaan kwakua hapendi kuwaona waja wa Allah wakiwa mbali na maasi.

  Tuna wajibu wa kufanya juhudi za kuwatoa katika hali zao kwa kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu na katika kubwa linaloweza kutusaidia katika jukumu hili ni dua njema kwao kwa maana kuwaombea kwa Allah awatoe huko na si kuwaombea dua za laana na maapizo wala kuwatusi.

 Sambamba na kutenda haya mlango wa kuchukia matendo yao mabaya upo pale pale na kuyachukia wanayo yafanya.   

                           Sheikh Abuu Fat’hiya Khamis kiza

Allah amhifadhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *