Ubora-wa-masiku-10-ya-mwanzoni-Dhulhijjah-4Pakua hapa
Mwongozo-wa-kuchinja-Udh-hiya-3-Pakua hapa
KUNUNUA-BAJAJI-KWA-MALIPO-YA-KIDOGOKIDOGOPakua hapa
Kiziwi-na-Bubu-waliofika-baleghePakua hapa
ufafanuzi-wa-makala-iliyopitaPakua hapa
MIAMALA-YA-RIBA-1Pakua hapa
TAHADHARI-DHIDI-YA-NJAMA-ZA-SHETANI-1Pakua hapa
Adhabu-za-Kaburini-1Pakua hapa

‏قال ابن مسعود رَضِيَ ٱللّٰهُ عَنْهُ:


Amesema Abdullah bin Mas’uud Allah amridhie:

« مادمت تذكر اللّه فأنت في صلاة ولو كنت في السوق ».


‘ Kwa muda ambao unamtaja Allah basi wewe upo katika swala hata kama utakua sokoni ‘

.

Kuna baadhi ya watu ambao wanaamini kwamba mkosi upo kwa watu au eneo, na wanadhani kwamba shari inaweza kuwapata kutoka katika maeneo hayo au watu hao moja kwa moja pasina hukumu ya Allah na makadirio yake. Na hii ndio imani ya mkosi ambayo Mtume swallallaahu alaihi wasallam ameikataza na akaeleza kuwa ni ushirikina. Kwa sababu mwenye imani ya mkosi anaamini kwamba kilichompata katika mabaya kinatoka kwa viumbe kama vile wakati au eneo au mtu, matokeo yake anamchukia mtu huyo au wakati huo au eneo hilo na anajitenga mbali nalo akidhani kwamba ndilo limemletea shari na anasahau au kujisahaulisha kuwa hakika kilichompata ni kutokana na hukumu ya Allah na makadirio yake na kwa sababu ya dhambi zake.