Categories
Nasaha za leo

FADHILA ZA KUWAPA NAFASI MAFUKARA

Amesema Mtume swallah Allahu alaihi wasalam:

ابغوني ضُعفائِكم، فإنما ترزقون وتنصرون بضُعفائِكم..

(( Nitafutieni wanyonge wenu , kwa hakika mnaruzukiwa na mnapewa ushindi kwa sababu ya wanyonge miongoni mwenu.))

وقال ابن معاذ رحمه الله :

Na akasema Ibnu Mu’adhi Allah amrehem:

: حبُّك الفقراء مِن أخلاق المرسلين، وإيثارك مجالستهم مِن علامات الصَّالحين، وفرارك منهم مِن علامات المنافقين

” Mapenzi yako kwa mafukara ni miongoni mwa tabia za mitume , Na kupendelea kwako kukaa nao ni katika tabia za waja wema , na kuwakimbia kwako ni katika alama za wanafiki. “

Nimesema :

” Katika hadith hii kuna kemeo la kuwa na kibri na msisitizo wa kuwa mnyenyekevu na mwenye kujishusha , Mtume swallah Allahu alaihi wasalam anawaeleza maswahaba zake wamtafutie wale wenye hali duni ili aweze kuwatekelezea haki zao ikiwemo kuwafanyia wema Je ni ipi hali yako na wanyonge katika watu wako wa karibu na jamii kwa ujumla ? umezitafuta hali na shida zao ? Hakika nusra ya Allah na ongezeko la rizki kwako ni kutokana na baraka za dua na shukran zao tafuta na jitoe kwa wenye uhitajio wa Mali na hali kwa manufaa yako kwanza kinyume na wanavyohisi wengi kuwa mnufaika ni mwenye kupokea.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *