Categories
Nasaha za leo

HII NDIO NEEMA KUBWA

Amesema Mtume swallah Allah ‘alaihi wasallam :

– مَن يُردِ اللَّهُ بهِ خَيرًا يُفقِّهُّ في الدِّينِ.

[ Allah akimtakia Mja wake kheri

humfahamisha katika dini ]‏

قال الشيخ عبد اللطيف بن عبد الرحمن آل الشيخ رحمه الله –

Amesema sheikh Abdul-latwiif bin Abdurrahman A’al sheikh Allah amrehemu :

أعظم منّة الله على مَن رزقه

الله معرفة الحق والاعتصام بكتابه.

“Neema kubwa ambayo Allah atamruzuku mja wake ni kuitambua haki na kushikamana na kitabu chake…

والتمسك بتوحيده

ووشرعه

Na kushikamana na tauhiid na kushikamana na sheria yake.”

Nimesema :

Ikiwa Allah amekujaalia kuikubali haki na kuipokea pale inapokufikia pasina kuwa na ugumu tambua umepata kheri kubwa na neema kubwa miongoni mwa neema za Allah.Na kinyume chake ukiona unakua na wepesi wa mambo ya kidunia na uzito katika kheri na kuifata haki basi hio ni shari kwako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *