Categories
Nasaha za leo

KILICHOKUWA BORA BAADA YA IBADA ZA FARADHI

‏قال الإمام الشافعي رحمه الله :


Amesema Imaam Shaafiy Allah amrehem :

ليس بعد أداء الفرائض،
شيء أفضل من طلب العلم .


Hakuna baada ya kutekeleza ibada za faradhi , kilichokua bora zaidi ya kutafuta elimu.


Nimesema :

Elimu ya kumtambua Allah na dini yake na Mtume wake swallah Allahu alaihi wasalam kuna nyakati inakua lazima na kuna nyakati inakua lazima kutokana na kile unachotakiwa kukisoma .

Muislam anawajibika kutenda ibada zake zote kwa Uono sahiih katika matendo na matamshi hivyo ni wajibu kwa kila muislam kujifunza itikadi yake na khaswa shahada mbili kutambua nguzo na masharti yake na yale yanayoweza kuibatilisha shahada yake.

Anawajibika kujifunza swala matamshi na matendo na kutambua katika matamshi hayo nguzo na wajibu na sunnah zake na hivyo hivyo katika baki ya ibada.

Na hata miamala ya kibiashara na kindoa pia aifanye kwa uono sahiih.

Tenga muda wa kuhudhuria halaqa za elimu ya dini zilizo katika mji wako na tenga muda wa kuskiliza darsa zinazo tumwa katika group zilizo nje ya mji wako

Hilo ndio jambo bora na lenye ujira mkubwa kwako baada ya ibada za lazima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *