Categories
Nasaha za leo

KWA DHIKRI HII UTAKUWA UMEMSHUKURU MOLA WAKO MLEZI

مَن قالَ حينَ يُصبِحُ: اللَّهمَّ ما أصبحَ بي من نِعمةٍ أو بأحدٍ من خلقِك فمنكَ وحدَك، لا شريكَ لَك، فلَك الحمدُ، ولَك الشُّكرُ، فقد أدَّى شُكرَ يومِه، ومن قالَ مثلَ ذلِك حينَ يُمسي، فقد أدَّى شُكرَ ليلتِه

Amesema Mtume swallallaahu alaihi wasallam : { Yeyote atakayesema pindi anapopambazukiwa na asubuhi; ” Ewe Allah sikuamka mimi nikiwa na neema yoyote , au yeyote katika waja wako (hakuamka akiwa na neema yoyote) isipokuwa imetoka kwako peke yako, na huna mshirika , basi sifa njema zote ni zako na shukrani zote ni zako “, Hakika (msemaji wa maneno hayo) atakuwa ametekeleza shukrani ya mchana wake wote. Na atakayesema mfano wa maneno hayo pindi anapofika jioni, hakika anakuwa ametekeleza shukrani ya usiku wake wote.}

Maelezo:

“Kumshukuru Allah aliyeneemesha ni katika mambo ya lazima na yenye kusababisha kuongezeka na kuduma kwa neema. Katika dhikri hii kuna kukiri neema kwa Allah pekee Aliyetakasika na Aliyejuu, na katika hilo kuna kukiri udhaifu na utegemezi wa mwanadamu kwa muumba, jambo ambalo ni sifa ya ukamilifu kwa mwanadamu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *