Categories
Nasaha za leo

MIONGONI MWA USIA WA MTUME SWALLAH ALLAH ALAIHI WASALLAM

Siku moja Mtume swallah Allah alaih wasalam alisema :

من يأخذ عني هؤلاء الكلمات فيعمل بهن، أو يعلِّم من يعمل بهن؟
  
Ni nani atakae chukua kwangu haya maneno ayafanyie kazi, au amfundishe atakae yafanyia kazi ?

قال أبو هريرة: قلت: أنا يا رسول الله، قال: 

Akasema Abu hurayra Allah amridhie : “Mimi ewe Mtume wa Allah” , Akasema Mtume swallallaahu alaihi wasallam:

اتق المحارم تكن أعبد الناس،

[ Yaogope aliyoyaharamisha Allah utakua mwenye kuabudu zaidi katika watu….,

وارض بما قسم الله تكن أغنى الناس،

Na ridhika na yale aliyokupa Allah utakua tajiri zaidi wa watu…,

وأحسن إلى جارك تكن مؤمناً،

Na mtendee wema jirani yako utakuwa muumin wa kweli..,

وأحب للناس ما تحبه لنفسك تكن مسلماً،

Na uwapendelee watu yale unayoyapenda kwa ajili ya nafsi yako utakuwa muislam wa kweli..,

ولا تكثر الضحك؛ فإن كثرة الضحك تميت القلب

Na Wala usikithirishe kucheka, hakika kukithirisha kucheka hufisha moyo…,

Maelezo kutoka kwa Mfasiri
Allah Aliyetukuka amuhifadhi:

Nimesema : Mtume swallah Allah alaihi katika nyasia alizotoa amefungamanisha kumtendea wema jirani kuwa ni miongoni mwa alama za imaan na kuwa hana imani yule ambaye jirani yake hasalimiki na maudhi yake.

Na pia Mtume wa Allah akatahadharisha kukithirisha kucheka na kuwa kitendo hicho hufisha moyo.

Mioyo yetu ina hali 3 – moyo ulio hai, moyo wenye maradhi na moyo uliokufa.

Aina hizi 3 za mioyo ndio msingi mkubwa wa Mja kuweza kusimama na kutekeleza ibada na kuweza kujikinga na Maasi.

Leo katika yaliochukua nafasi kubwa ni sisi kukithirisha kucheka na kuangalia au kusikiliza vyenye kuchekesha.

Katika simu zetu badala ya kunufaishana, baadhi ya watu wao ni kutafuta sababu za kucheka na mengi ni ya kipuuzi na mengine mengi yamekua ni yenye kuifanyia mzaha dini ya Allah.

Huenda kwa kufanya hayo mioyo hufa au kuwa na maradhi ya kutoipokea na kuifanyia kazi haki.

Tunamuomba Allah salama na afya katika nyoyo zetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *