Categories
Nasaha za leo

MUONGOZO MUHIMU

MUONGOZO

Huu ni muongozo muhimu saana katika kunukuu khabari:-

Si kila unalosikia husemwa.

Amesema Mtume swallah Allah alaih wasallam:-

كفى بالمرء كذبا أن يحدث بكل ما سمع

(( Inamtosheleza Mtu kuwa muongo kwa kuhadithia kila anacho kisikia ))

Na ikaja katika mapokezi mengine :

(( Inamtosha Mtu kupata madhambi kwa kusema kila anacho kisikia ))

Amesema imaam Maalik Allah amrehem :-

اعلم أنه فساد عظيم أن يتكلم الإنسان بكل ما سمع

(( Tambua hakika uharibifu mkubwa ni Mtu kuzungumza kila anacho kisikia. ))

السير للذهبي 8/66

Nimesema :-

Katika yale tunayo yasikia yapo ya kweli na yapo yasiokua ya kweli hivyo ikiwa utakua na utaratibu wa kuzungumza kila unacho kiskia huwezi kusalimika na uongo na mwenye akili anatambua si kila analosikia husemwa na sio kila analolijua hufaa kuenezwa.

Na khaswa katika zama zetu watu tumekua na wepesi wa kueneza khabar na kwa haraka pasina kupima usahiih wake na je linafaa kusemwa japokua ni sahiih na je mimi ni muhusika wa kulisema hili ?

Hayo ni mambo muhimu saana katika kuichunga heshima yako na kutoleta tashwish katika jamii na tufaham kuwa maneno ni katika matendo yetu kwayo tutahesabiwa nayo na kulipwa kheri na shari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *