Categories
Nasaha za leo

Nasaha

‏قال الشيخ صالح الفوزان -حفظه الله-:
Amesema Sheikh swaaleh Alfawzaan Allah amhifadhi :

عمر الإنسان أيام معدودة فما دمت معافا في بدنك وفي أمن واستقرار فسارع إلى الاشتغال بالطاعات.
Umri wa mwanadamu ni masiku yenye kuhesabika basi kwa muda ambao umesalimika katika mwili wako , na upo katika amani , na utulivu basi fanya haraka kushughulika na twaa ya Allah

📚شرح كتاب الكبائر (565)

Nimesema :
Uhai wako ndio rasilimali yako , bali muda wako ndio kitu ghali na chenye thamani kubwa katika maisha yako lakini ndio katika vitu visivyo tiliwa umuhimu kabisa na rahisi kupotezwa

Nyakati zina potezwa katika mazungumzo yasio na faida katika maskan nyingi , Nyakati zinapotezwa katika Ma TV na masaa kwa masaa hupotezwa pasina kutajwa Allah wala kufanywa twaa

Na jambo kubwa linaloweza kukusaidia kutumia muda wako vyema ni kutambua kuwa kifo huja ghafla na kitakata hali yako ya kutenda hivyo patiliza Uhai wako.

Abu fat’hiyah khamis kiza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *