Categories
Makala Nasaha za leo

QUR AN NI NURU

Amesema Mtume swallah Allahu alaihi wasalam :
عليْكَ بِتِلاوةِ القُرْآن، فإنّهُ نورٌ لكَ في الأرضِ، وذُخرٌ لكَ في السّماء.
Ni juu yako kulazimiana na kuisoma Quraan, hakika ni nuru kwako katika ardhi ( dunia ) na ni limbikizo kwako mbinguni ( akhera )
📚صحيح الترغيب (1422)

و‏قال الامام الشافعي – رحمه الله -:
Na amesema Imaam Shaafiy Allah amrehem :

وطَلبنَا ضِياءَ القُبُورِ فَوَجَدنَاهُ في قِراءةِ القُرآن.
Na tulitafuta nuru ya (Maisha ya) kaburini , tukaipata katika kuisoma Quraan

📕- [ البُحور الزاخرة (١/١٨٥)

Maisha ya sehem hizi tatu yapo na hayana namna tofauti, maisha ya hapa duniani ambayo ndio sehem ya maisha ya Barzakh (baada ya kufa kaburini mwetu sawa tuzikwe au laa) na maisha ya baada ya kufufuliwa siku ya kiyama

Ukitaka maisha yako ya sehem hizi tatu yawe na nuru basi ni juu yako kukithirisha kuisoma Quraan

Je Quraan ina ratiba katika maisha yako ya kila siku, kujifunza na kuisoma na kuihifadhi na kuifanyia kazi?

Yatie nuru maisha yako kwa kukithirisha kuisoma Quraan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *