Categories
Makala

SHAABAN MWEZI WA SWAUM

Haifichiki kwa mwenye akili kuwa dunia ni sehem ya maandalizi ya maisha ya akhera , na si pahala pa kudumu kwa kila chenye uhai

Masiku yanakwenda na kukatika rasilimali ya kuchuma kwa ajili ya maisha ya akhera nayo ni umri , masiku yaliopita hubakia kama ndoto tu na masiku yajayo hubakia katika matarajio na muda uliopo usipo makinika utapotea na kubakia kuishi katika ndoto na matarajio juzi tu tumemaliza Ramadhan na Leo hii ramadhan ipo mbele yetu basi tutumie vyema fursa ya Umri wetu.

Shaaban ni mwezi wa maandalizi ya ramadhan na katika maandalizi hayo ni kukithirisha kufunga.

Imekuja katika hadith ya Aisha Allah amridhie amesema :
لَمْ أَرَهُ صَائِمًا مِن شَهْرٍ قَطُّ، أَكْثَرَ مِن صِيَامِهِ مِن شَعْبَانَ كانَ يَصُومُ شَعْبَانَ إلَّا قَلِيلًا..
sikumuona Mtume wa Allah akifunga katika mwezi kamwe zaidi ya funga yake katika mwezi wa Shaaban , Alikua Mtume akifunga shaaban ispokua masiku machache

Imepokewa na imaam Muslim.

Sababu ya kukithirisha kufunga ndani ya Mwezi huu wa Shaaban

Aliulizwa Mtume swallah Allah alaihi wasalam :

ذلِكَ شَهْرٌ يَغفُلُ النَّاسُ عنهُ بينَ رجبٍ ورمضانَ ،
Huo ni mwezi ambao wanaghafilika watu ulio kati ya rajab na ramadhan
وَهوَ شَهْرٌ تُرفَعُ فيهِ الأعمالُ إلى ربِّ العالمينَ ، فأحبُّ أن يُرفَعَ عمَلي وأَنا صائمٌ.
Nao ni mwezi ambao matendo hupandishwa kwa mola mlezi wa walimwengu nami hupenda matendo yangu yapande nikiwa nimefunga .

hadith imepokewa na imaam Nasaai kutoka kwa Usama bin zaidi

Shaaban ni mwezi ambao matendo hupandisha kwa Allah subhaana wataala kwani matendo hupandishwa kwa Allah kwa siku , kwa wiki na kwa mwaka na shaaban ni matendo ya mwaka na Alkhamis ni matendo ya wiki

Amesema Ibn Uthaimin Allah amrehem:
أما شعبان فنعم يمتاز عن غيره بأن النبي ﷺ كان يكثر صومه. بل كان يصومه كله إلا قليلاً.
Ama shaaban ndio hujipambanua na miezi mingine kwakua Mtume swallah Allahu alaihi wasalam akikithirisha kuifunga , bali alikua akifunga shaaban yote ispokua siku chache
فينبغي الإكثار من الصيام في شعبان.
Inatakikana kukithirisha kufunga katika mwezi wa shaaban
📕الباب المفتوح 174

Abu fat’hiyah khamis kiza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *