Categories
Taarifa

TANGAZO KUHUSU FURSA ADHIMU YA KUSOMA DINI

Uongozi wa Markaz Ibnu Uthaymin unawatangazia waislamu wote kuhusu uanzishwaji rasmi wa masomo ya taaluma ya dini katika mwaka huu wa msomo 1444 – 1445H sawa na 2023 – 2024M. Sambamba na matangazo kadha wa kadha yaliyotolewa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano kuhusu fursa hii, hili ni tangazo la kuanza masomo yetu rasmi kwa vijana ambao tayari tumeshawapata kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Ratiba yetu ya masomo inaanza ndani ya wiki hii inayoanza leo (20/5/2023) kwa vipindi vya asubuhi mpaka mchana kwa kiwango cha Tamhiidi na Mutawasitwa. Fursa hii inaambatana na ile ya kuhifadhisha Qur’an Tukufu kwa rika la vijana wa kiume na wa kike.

Bado hujachelewa mlete mwanao afaidike kwa kupata elimu ya kumtambua Mola wake Mlezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *