Categories
Maswali na Majibu ya Wanachuoni Maswali ya Tauhidi

UHUSIANO KATI YA TAUHIDI NA IMANI

Aliulizwa Sheikh Ibnu Uthaymin Allah amrehemu: Je Tauhidi ndio Imani?

Akajibu:

الإيمان والتوحيد شيئان متغايران وشيئان متفقان، فالتوحيد هو إفراد الله عز وجل بما يستحقه ويختص به من الربوبية والألوهية والأسماء والصفات، ولهذا قال العلماء رحمهم الله: إن التوحيد ينقسم إلى ثلاثة أقسام: توحيد الربوبية، وتوحيد الألوهية، وتوحيد الأسماء والصفات. وإن هذه الأقسام جاءت في قوله تعالى: (رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيّاً) . فقوله: (رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا) يعني توحيد الربوبية، وقوله: (فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ) يعني توحيد الألوهية، وقوله: (هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيّاً) يعني توحيد الأسماء والصفات. وهذا التقسيم للإيمان في الواقع؛ لأن الإيمان بالله عز وجل يتضمن الإيمان بربوبيته وألوهيته وأسمائه وصفاته، وعلى هذا فالموحد لله مؤمن به، والمؤمن بالله موحد له، لكن قد يحصل خلل في التوحيد أو في الإيمان فينقصان، ولهذا كان القول الراجح أن الإيمان يزيد وينقص، يزيد وينقص في حقيقته وفي آثاره ومقتضياته: فالإنسان يجد من قلبه أحياناً طمأنينة بالغة، كأنما يشاهد الغائب الذي كان يؤمن به، وأحياناً يحصل له شيء من قلة هذا اليقين الكامل، وإذا شيءت أن تعرف أن اليقين يتفاوت فاقرأ قول الله تعالى عن إبراهيم خليله عليه الصلاة والسلام: (وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَى قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِنْ قَالَ بَلَى وَلَكِنْ لِيَطْمَئِنَّ قَلْبِي) . كما أنه أيضاً يزيد بآثاره ومقتضياته: فإن الإنسان كلما ازداد عملاً صالحاً ازداد إيمانه، حتى يكون من المؤمنين الخلص

Imani na Tauhidi ni vitu viwili vinavyotofautiana na pia vinaafikiana. Tauhidi ni kumpwekesha Allah katika yale yote ambayo anastahiki na yanayomuhusu yeye pekee kama vile ulezi wa viumbe na uabudiwa na majina yake na sifa zake. Na kwa sababu hiyo wamesema wanachuoni Allah awarehemu; hakika Tauhidi inagawanyika katika aina tatu:-

  • Upekee wa Allah katika ulezi wake (Tauhidi ya Ulezi).
  • Upekee wa Allah katika kuabudiwa kwake (Tauhidi ya ibada).
  • Upekee wa Allah katika majina yake pamoja na sifa zake (Tauhidi ya majina na sifa za Allah).

Na imekuja aya ifuatayo kwa ajili ya mgawanyo huu:{Mola mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, basi muabudu yeye tu na usubiri katika ibada yake, je unamfahamu mwenye majina kama yake?}; Aliposema (Mola mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake) anakusudia Upekee wake katika Ulezi (Tauhidi ya Ulezi), na aliposema (basi muabudu yeye tu na usubiri katika ibada yake) anakusudia Upekee wake katika kuabudiwa (Tauhidi ya Ibada), na aliposema (je unamfahamu mwenye majina kama yake?) anakusudia Upekee wake katika majina yake na sifa zake (Tauhidi ya Majina na sifa zake). Na huu ndio mgawanyo wa imani kwa uhalisia wake; kwa sababu imani ya kumuamini Allah inaambatana na kuamini Upekee wake katika Ulezi wake na Kuabudiwa kwake na Majina yake na Sifa zake. Kwa ajili hiyo , mwenye kumuamini Allah ndiye mwenye kumpwekesha Allah na mwenye kumpwekesha Allah ndiye muumini.
Lakini inaweza kupatikana dosari katika Tauhidi ya mtu au katika imani yake , vikawa viwili hivyo vimepungua kwake, na kwa sababu hiyo, kauli iliyokuwa na nguvu ni kwamba imani ya mtu huzidi na hupungua . Huzidi na hupungua katika uhalisia wake kabisa na katika athari yake na matokeo yake: (mfano), Mwanadamu baadhi ya nyakati huwa anakuta moyoni mwake kuna utulivu wa hali ya juu imani , kiasi ambacho huwa kama anatazama kwa macho yale mambo yaliyofichikana kwake katika miongoni mwa yale anayoyaamini moyoni mwake , na wakati mwingine hupungua kiasi fulani cha yakini hii kamilifu (ya moyoni mwake).
Na ukitaka kufahamu kwamba hakika yakini ya imani hutofautiana, basi soma kauli ya Allah kuhusu Ibrahimu kipenzi chake, amani iwe juu yake :{Na kumbuka pindi aliposema Ibrahimu ewe Mola wangu Mlezi nionyeshe namna unavyohuisha wafu, (Allah) akasema, Je huamini? (Ibrahimu) akasema, hapana! bali ili moyo wangu utulizane }. Vilevile imani huzidi kwa athari na matokeo yake (mfano), hakika mwanadamu kila napoongeza matendo mema ndivyo imani yake huzidi, mpaka nakuwa miongoni mwa waumini halisi.





Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *