Categories
Maswali ya Tauhidi

WATU WA TAUHIDI NI WATU GANI?

Aliulizwa Sheikh Ibnu Uthaymin Allah amrehemu swali lifuatalo:

Nilisoma katika kitabu fulani kwamba watu wa Tauhidi (ikiwa wataingia motoni) hawatokalishwa motoni milele (bali watatolewa na kuingizwa peponi). Je ni akina nani hao watu wa Tauhidi? “

Akajibu ;

أهل التوحيد الذين عبدوا الله تعالى وحده، الذين عبدوا الله تعالى وحده أي: قاموا بالعبادة مخلصين بها لله، متبعين فيها لرسول الله صلى الله عليه وسلم، هؤلاء هم أهل التوحيد، ولا يختصون بطائفةٍ دون أخرى، في أي بلادٍ كان الإنسان، ومن أي قبيلةٍ كان، ومن أي جنسٍ كان، إذا قام بعبادة الله عز وجل وحده، متبعاً في ذلك رسوله صلى الله عليه وعلى آله وسلم فهو من أهل الجنة

[[ Watu wa Tauhidi ni wale ambao wanamuabudu Allah Mtukufu peke yake (bila ya kumshirikisha na chochote) na wamesimama imara katika kuabudu kwao kwa kumtakasia yeye tu ibada zao, wenye kufuata mwenendo wa Mtume wa Allah swallallaahu alaihi wasallam katika hilo , hao ndio watu wa Tauhidi. Wala si kikundi maalumu cha watu kinyume na kikundi kingine wala si watu wa nchi maalumu bali nchi yoyote atakayokuwepo na kabila lolote atakalokuwa nalo na jinsia yoyote aliyonayo ikiwa tu atasimama imara katika kumuabudu Allah Mtukufu peke yake na akamfuata Mtume swallallaahu alaihi wasallam katika hilo, basi huyo ni mtu wa peponi. ]]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *