Categories
Nasaha za leo

WEMA WALIOTANGULIA WALIVYOISHI NA WATUMISHI WAO

دخل رجل على سلمان الفارسي رضي الله عنه وهو يعجن!

فقال: ما هذا يا أبا عبدالله؟


Aliingia bwana mmoja kwa Sulaymaan Al-faarisiy Allah amridhie akamkuta akiwa anakanda unga , akasema : Kipi hiki ewe baba Abdullah ( kwa kipi unafanya kazi mwenyewe ) ?

قال: بعثنا الخادم في عمل فكرهنا أن نجمع عليه عملين


Akasema : “Tumemtuma mfanyakazi wetu katika kazi fulani na tukachukizwa kumkusanyia juu yake kazi mbili.”

Nimesema :

Hivi ndivyo walivyokuwa wema waliotangulia na watumishi wao , wakiwapa nafasi ya udugu na kuwafanyia muamala wa upole bali na kuwasaidia majukumu, nasi tunasema kama alivyosema Mtume wa Allah kuwaambia waliopewa nafasi ya kuwa na wasaidizi wa kazi :

Hawa ni ndugu zenu na Allah amewajaalia kuwa mikononi mwenu , msiwape kazi wasizo ziweza na mkiwapa kazi basi wasaidieni. “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *